Najiamini Animation Launch Press
Release

Tai Tanzania, in partnership with the Canadian Embassy, is acknowledging and celebrating this year’s International day of people with disabilities by introducing a new 3D animation, Najiamini, created with the community for the community. In alignment with this year’s theme, “Transformative solutions for inclusive development: the role of innovation in fuelling an accessible and equitable world,” Tai Tanzania pioneers the use of storytelling for social change. A new innovative approach to changing the behaviours and mindsets of our community which are not beneficial to us. Najiamini is being used to encourage young people living with disabilities, to advocate for the infrastructural needs of students with disabilities and to raise awareness on the challenges faced by young people with disabilities and how we can all be a part of the solution.  

Najiamini is a story inspired by real-life events showcasing the struggles of, Mira, a girl who loves basketball and lived most of her life without a disability but became disabled after a tragic accident. Faced with a physical disability, her dreams of becoming a professional basket player seemed far fetched. With the lack of infrastructure to support students with disabilities and stigma and bullying, Mira strived to rise above all odds. The support she received from her close friends and family and her self-motivation allowed her to dream again. Her dream was to make it to the Paralympics and represent her country in wheelchair basketball – she made it!   

Created hand in hand with various leaders and advocates of people living with disabilities, Najiamini is a well-researched animation film being launched on the 2nd of December 2022. Additionally, the launch of the film is honoured to host various members of the Shiyawata Community, the National Wheelchair Basketball Team and have the High Commission of Canada, Mr Kyle Nunas, and special guests Mr Ipyana Mwaipaja, City Cultural Officer and Mark Bryan, the Representative of UNFPA Tanzania.   

We believe it is necessary to use more innovative ways to impact our community positively and to ensure we are fuelling an accessible and equitable world.  

Follow us on our social media pages @taitanzania on Instagram, Twitter and Facebook and watch Najiamini on our YouTube page, “Tai Studio”.  

Uzinduzi wa Filamu Ya Najiamini 

Tai Tanzania, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Kanada, inatambua na kuadhimisha siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu ya mwaka huu kwa kutambulisha katuni chapa tatu mpya iitwayo Najiamini. Najiamini umeandaliwa kwa ajili ya jamii yetu ya Tanzania. Kwa kuzingatia kaulimbiu ya kitaifa ya mwaka huu, “Suluhisho kuu la maendeleo jumuishi: jukumu la uvumbuzi katika kuchochea ulimwengu unaofikiwa na wenye usawa,” Tai Tanzania ni taasisi iliyoweka kipaumbele kwenye matumizi ya hadithi kwa mabadiliko ya kijamii. Mbinu mpya bunifu ya kubadilisha tabia na mawazo hasi ya jumuiya yetu. Filamu ya Najiamini inatumiwa kuhimiza vijana wanaoishi na ulemavu, kutetea mahitaji ya miundombinu ya wanafunzi wenye ulemavu na kuongeza uelewa juu ya changamoto zinazowakabili vijana wenye ulemavu na jinsi sote tunaweza kuwa sehemu ya suluhisho. 

Najiamini ni hadithi iliyochochewa na matukio halisi yanayoonyesha mapambano ya, Mira, msichana ambaye anapenda mpira wa vikapu na alizaliwa bila ulemavu lakini akawa mlemavu baada ya ajali akiwa mwanafunzi. Mira aliona ndoto zake zikififia mbele ya macho yake. Kwa ukosefu wa miundombinu ya kusaidia wanafunzi wenye ulemavu na unyanyapaa na uonevu, Mira alijitahidi kushinda vikwazo vyote. Usaidizi aliopokea kutoka kwa marafiki zake wa karibu na familia pamoja na ari yake binafsi ilimruhusu kutokukata tamaa. Ndoto yake ilikuwa kufika kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu na kuwakilisha nchi yake katika mpira wa vikapu wa viti vya magurudumu – alifanikiwa! 

Filamu hii ya Najiamini imeandaliwa kwa ushirikiano wa viongozi mbalimbali na watetezi wa watu wanaoishi na ulemavu. Ni filamu ya uhuishaji iliyofanyiwa utafiti na kuzinduliwa tarehe 2 Desemba 2022. Zaidi ya hayo, uzinduzi wa filamu hiyo imepata bahati ya kuzinduliwa na wanachama mbalimbali wa Jumuiya ya Shiyawata, Kocha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Viti vya Magurudumu na Balozi wa Kanada, Bw Kyle Nunas, pamoja na wageni maalum Bw Ipyana Mwaipaja, Afisa Utamaduni wa Jiji na Bw Mark Bryan, Mwakilishi wa UNFPA Tanzania. 

Tunaamini ni muhimu kutumia njia bunifu zaidi ili kuathiri vyema taifa letu na kuhakikisha kuwa tunachochea ulimwengu unaofikiwa na usawa. 

Tufuate kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii @taitanzania kwenye Instagram, Twitter na Facebook na utazame Najiamini kwenye ukurasa wetu wa YouTube, “Tai Studio”.